Shahidi Mkuu wa Mauaji ya Kevin Omwenga Apatikana Ameuawa Nyumbani Kwake
Wycliffe Omwenga, kaka yake mfanyabiashara Kevin Omwenga, ambaye aliuawa mwaka 2020, na shahidi mkuu wa kesi hiyo ya mauaji amepatikana amefariki. Ripoti ya polisi ilisema mwili wa Wycliffe ulipatikana Jumatano, Julai 21, nyumbani kwake Riruta, Nairobi lakini bado hawajabainisha chanzo cha kifo chake.