COVID-19 Yawaangamiza Wagonjwa 6, Watu 723 Wanasa Virusi
Watu 723 wamethibitishwa kunasa Covid-19, kutokana na sampuli 6,881 zilziopimwa katika saa 24 zilizopita na kusukuma idadi ya maambukizi kenya 192,435. Asilimia mpya ya maambukizi ya corona nchini ni 10.5% huku jumla ya chanya zilizopimwa tangu mwezi Machi kisa cha kwanza kuripotiwa nchini ikugonga 2,050,236.