Shida ya Ruto ni handisheki, Raila asema kuhusu matatizo ya Jubilee

Posted by Martina Birk on Monday, September 23, 2024

- Raila amesema matatizo ya Jubilee ni viongozi ambao hawataki handisheki kati yake na Rais Kenyatta

- DP Ruto na wafuasi wake wamekuwa wakiuliza maswali chamani kuhusu mabadiliko ya maafisa wa kamati ya kitaifa

- Raila aliongeza kuwa Wakenya wataingia kwenye mchakato wa refarenda mara tu janga la covid-19 litakabiliwa

Kinara wa ODM Raila Odinga amesema matatizo ambayo chama cha Jubilee kinapitia ni kwa sababu Naibu Rais William Ruto amekataa kukubali handisheki.

Raila walifanya mwafaka wa handisheki na Rais Uhuru Kenyatta Machi 9, 2018 akisema lengo ni kuwaunganisha Wakenya.

Habari Nyingine: Coronavirus: Runinga ya Citizen yalazimika kumuomba Rais Magufuli msamaha

Akiongea kwenye mahojiano na redio ya Namlolwe, Raila alisema shida kubwa ya Jubilee ni baadhi ya viongozi ambao hawana haja na maslahi ya Wakenya.

Handisheki yangu na rais ilikuwa ya kuwaunganisha Wakenya. Lakini, kuna baadhi ya watu ndnai ya Jubilee ambao wanaipinga na hiyo ndio chanzo cha masaibu ya chama hicho," alisema Raila.

"Baadhi ya viongozi wa Jubilee hawana haja na matatizo wanayopitia Wakenya, wanaangazia tu 2022," aliongeza.

Habari Nyingine: Wakili 'Grand Mullah' apuuzilia mbali mchakato wa Kagwe katika kupamana na Covid-19

Aidha kiongozi huyo alisema kwa sasa anaangazia vita dhidi ya coronavirus na baada ya kukabiliwa Wakenya wataenda kwenye mchakato wa kura ya maamuzi.

"Tunataka kuangazia kwanza na janga la coronavirus kwa sasa ndio baadaye tushiriki refarenda," alisema Baba.

Raila pia alisema mkutano wake na katibu mkuu wa muungano wa wafanyikazi nchini Cotu Francis Atwoli, waziri Eugene Wamalwa, naibu mwenyekiti wa Jubilee David Murathe na wandani wake James Orengo na Junet Mohammed Aprili 13 haukuwa wa kujadili siasa.

Habari Nyingine: Binti mfalme wa Sweden ageuka mhudumu wa afya ili kusaidia kupigana jinamizi la coronavirus

Kiongozi huyo aliyasema hayo wakati ambapo Jubilee imekumbwa na misukosuko kuhusiana na mabadiliko ya wanachama katika kamati ya kitaifa ya chama (NMC).

DP Ruto aliwaka moto kwenye mitandao baada ya kupata habari kuwa kuna maafisa ambao tayari wamependekezwa kuchukua nafasi hizo.

Alisema kuna wakora ndani ya chama ambao wanapanga njama za kufanya mabadiliko chamani kupitia milingo ya nyuma.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdjan9zfZhmqqGhlJZ6uq2Mq6ytp12jtm60wKeboquYmriqedGaoKWZXZbAprnAZqKuoKWowm65wK2YraGqpHq6rYyjrJuhnJqyb7TTpqM%3D