Maafisa wa Polisi Kaunti ya Garissa wamethibitisha kuwa Wakenya wawili ambao walikuwa wametekwa nyara na kundi la kigaidi la al-Shabaab wamepatikana na kuokolewa.
Abdulahi Isaack Harun na Abdi Hassan Ilkaase walitekwa nyara siku ya Alhamisi, Desemba 26, wakati walikuwa safarini kuelekea Liboi.
Habari Nyingine: Serikali yamtolea wakili Miguna masharti makali kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini
Habari Nyingine: Mshukiwa wa mauaji ajifanya mwenda wazimu kortini kuhepa kujibu mashtaka
Kulingana na ripoti ya polisi mnamo Jumapili, Desemba 2019, wawili hao hawakujeruhiwa na wako katika hali nzuri kiafya licha ya kuonekana kuwa wachovu.
"Hii ni kuthibitisha kuwa Abdullahi Issack Harun na Abdihassan (Ilkaase) ambao walikuwa wanasafiri wakitumia gari aina ya landcruizer KCM 446R ambalo linadaiwa kutekwa nyara na wanachama wa kundi la al-Shabaab wamepatikana na wamewasili kituoni hii leo 29/12/2019 huku wakiwa katika hali nzuri kiafya japo ya kuonekana wachovu," ilisoma sehemu ya ripoti hiyo.
Habari Nyingine: Roselyn Akombe: Msando aliuawa kwa kulinda maadili ya uchaguzi
Mafisa hao wa usalama walitambua kuwa wawili hao walitekwa nyara na wanachama 20 wa kundi hilo la kigaidi lakini ni watatu pekee miongoni mwao ndio waliandamana na waathiriwa nchini Somalia katika eneo la Bagdad
"Walikabithiwa begi ambazo zinaonekana kuwa radio ama GPRS na ni wanachama watatu pekee wa al-Shabaab waliandamana na waathiriwa Somalia katika eneo la Bagdad,kilomita 60 kutoka Hosingo ambao wamekita kambi yao na kuweka bendera nyeusi," ilisoma ripoti hiyo .
Wawili hao waliwachiliwa huru siku ya Ijumaa, Desemba 27, mwendo wa saa kumi jioni.
Polisi wameomba umma hususan wakazi wa Liboi kuwa makini kwani wanachama 15 wa kundi la al-Shabaab bado wamekita kambi eneo hilo.
"Ni dhahiri kuwa wengine ambao walikuwa zaidi ya wanachama 15 wa al-Shabaab walisalia Liboi, Walburat na bwawa la Daddquranna wanapanga kuteka vilipuzi vya IED katika kambi za polisi, kufumania gari la polisi na kuwavamia wanao safiri kwa mabasi. Kuna haja ya kushika doria ya asasi tofauti kukabiliana nao," ilisoma ripoti hiyo ya polisi.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaH90fZJmnpqqmajAonnWmqKepqmWenN51pqjoqebqsSiedaapJ6slaDEonnNspirmV2jrm6ty2aqoZmSlq6jedaapqSnnJrEonrHraSl