- Tharaka Nithi ilijaza kikapu cha Kibaki 2007 lakini hezabu ya wakazi imeonyesha wako chini
- Mbunge Chepkut alisema hilo linaonyesha kumekuwa na wizi wa kura
- Hata hivyo mwandani huyo wa DP ruto alilazimika kufuta ujumbe huo baadaye
Mbunge wa Ainabkoi William Chepkut Jumanne,Novemba 5, alilazimika kufuta ujumbe wake kwenye Twitter baada ya kusema kuwa uushindi wa kinara wa ODM Raila Odinga kwenye kinyang'anyiro cha urais umekuwa ukiibwa.
Chepkut alisema hilo baada ya matokeo ya hesabu kamili ya Wakenya katika kila kaunti iliyotolewa.
Habari Nyingine: Picha za kutamanika za muigizaji wa kipindi cha Maria Brian Ogana almaarufu Luwi
Mbunge huyo alisema hilo kutokana na idadi ya watu katika kaunti ya Tharaka Nithi ambpo hesabu hiyo ilionyesha kaunti hiyo ina watu 393,177.
Mnamo mwaka wa 2007, ambapo Raila walikuwa wakishindana na Mwai Kibaki, kaunti hiyo ilipiga vichwa vya habari baada ya kujaza kikapu cha Kibaki kwa naomna iliyoshangaza.
Wakati huo kura zilikuwa zikihesabiwa na kuonyesha Raila alikuwa akiongoza pakubwa kabla ya kaunti hiyo kutoa kura takriban 216, 000.
Habari Nyingine: Mtahiniwa wa KCSE akataa kufanya mtihani, adai hajajiandaa vilivyo
Baada ya kura za Thharaka Nithi kuingia, Kibaki alipunguza pakubwa tofauti kati yake na Raila na mwishowe kuishia kuwa mshindi.
"Kitu kimoja nimeona na hesabu ya Wakenya ni kuwa Raila Odinga amekuwa akishinda urais lakini njama ya kuibwa kwa ushinda wake imekuwa kali. Ama ni vipi utaelezea kuhusu matokea ya idadi ya Wakenya kwenye maeneo kama vile Tharaka Nithi iliyojulikana kwa idadi kubwa lakini inaonekana ni wachache!" Mbunge huyo alisema.Hata hivyo, baada ya muda alifuta ujumbe huo lakini TUKO.co.ke ilikuwa tayari imeupata .
Habari Nyingine: Wavinya Ndeti awaka moto kufuatia matamshi ya Raila Odinga kuhusu wanawake wa Ukambani
Matokeo ya uchaguzi huo wa 2007 yalizua machafuko ya kikabila baada ya Raila kusema kura zake zilikuwa zimeibwa na akawataka wafuasi wake kuandamana kudai haki.
Hali hiyo imesababisha mwafaka wa kisiasa ambapo aliyekuwa katibu wa Umoja wa Mataifa wakati huo Koffi Annan aliwapatanisha Kibaki na Raila.
Wawili hao waliishia kuunda serikali ya mseto maarufukama nusu mkate.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZ4BxfJZmpJutnpyybq3LmrGipZmgrm631J%2BsrZldqre2ucGeZKSvlaPGpnnTsKCtrJWneqOtwJ2YZrGRYri2v8SmmGaqkZ65onnApaCsoJmjsaJ51Jyfmp%2Blr7ZvtNOmow%3D%3D