-Haji alisema kuwa alipokea vitisho vya kuuawa kutokana na vita vyake dhidi ya wahusika wa ufisadi wenye ushawishi
-DPP alisema kuwa amezoea vitisho tangu kikundi cha magaidi cha al-Shabaab na Al-Qaeda alipokuwa wakala wa upelezi wa taifa
-Haji alisema kuwa vitisho vimetolewa kwa familia yake lakini alisema hatatishwa
-DPP alisema watu kutoka sekta tofauti wamemuunga mkono na kusisitiza kutiwa mbaroni kwa washukiwa siku za Ijumma kutaendelea ikiwa kuna sababu ya kufanya hivyo
Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma (DPP) Noordin Mohamed Haji amesema kuwa vitisho vya mauaji havitamzuia kukabiliana na ufisadi nchini bila kuzingatia nyadhifa za wahusika na mali walio nayo.
Haji ambaye awali alikuwa afisa wa upelelezi (NIS) alisema kuw amewahi kupokea vitisho kutoka kwa al-Shabaab na Al-Qaeda, hivyo hawezi kuogopa vitisho vyovyote katika kazi yake.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine: Video ya maafisa wa polisi wakicheza 'Kwangwaru' ya Diamond yawaacha Wakenya vinywa wazi
Habari Nyingine: Mama avua nguo nje ya ofisi ya Uhuru kulalamikia 8% VAT (picha)
“Nimepokea vitisho kutoka kwa vikundi vya kigaidi nilipokuwa ajenti wa NIS, hivyo hakuna kitu kipya. Familia yangu pia imepata vitisho kutoka kwa al-Shabaab. Wengine wamejaribu kumhusisha babangu kwenye kesi ya tume ya kitaifa ya ardhi kunitatiza, lakini ninajua na nitaendelea kuwa mwadilifu kwa kazi yangu,” Haji alisema.
Haji alishangaa kwa nini babake ambaye alikuwa waziri wa zamani wa usalama na seneta wa sasa wa Garissa Yusuf Haji alihusishwa kwenye kesi hiyo ya tuma ya kitaifa ya ardhi baada ya washukiwa wote kwenye kesi hiyo kushtakiwa.
Habari Nyingine: Watoto wa China sasa wanaimba Kiswahili kuliko Wakenya, tazama video
Alisema kuwa kuhusishwa kwa babake kwenye kesi hiyo kulitumiwa kumwonya kulegeza Kamba kwenye vita dhidi ya ufisadi.
“Iwe wazi kwa kila mtu kuwa ninaamini Mungu ndiye mkuu atayeelekeza siku zangu za usoni. Tarehe aliyopanga nife haiwezi kubadilika. Sitaogopa ikiwa mwelekeo nitakaochukua utanisababishia mauti. Itaniridhisha sana. Ninataka kufanya mambo mazuri zaidi kwa Mungu na kwa taifa langu,” Haji aliongeza.
Habari Nyingine: Masharti 10 ya kuzingatia ukiwa na uhusiano na ‘sponsor’
Haji amesifiwa sana kwa kuongeza kasi na ukakamavu kwenye vita dhidi ya ufisadi huku Rais Uhuru Kenyatta akimtegemea kuendeleza vita hivyo na kuziba mianya ya ufisadi.
“Ninatumai nitapata matokeo mazuri na nitafanya kazi yangu kwa unyenyekevu kwa kuwa ni heri njema kutoka kwa sekta muhimu kumaliza athari za ufisadi,” Haji alisema.
Haji alisema kuwa ataagiza watu wanaoshukiwa kuhusika kwenye ufisadi na kuwa watu maarufu wanaolalamikia kutiwa mbaroni kwa washukiwa siku za Ijumaa sio tofauti na watu wanaokamatwa siku zingine za wiki.
Read ENGLISH VERSION
Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News
Bibi Cecilia aliye gwiji wa kutengeneza mifumo ya muziki apata meno mapya | TUKO TV
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibYR1fY9mn5qskWLDqsDIrJ%2BoZaaurm63yJ%2BmZqCRq7a4sdmiZKStnp7HtrXAZqKuqJGir6K6wGalmmWlm7a0rcOiZJ2ooGK7sLvRnaCnZZiWt6p6x62kpQ%3D%3D