-Mahakama imeagiza kuwa mshukiwa wa utapeli Benson Wazir Chacha mwenye umri wa miaka 23 afanyiwe uchunguzi wa kiakili katika hospitali ya watu wenye akili punguani ya Mathari
-Mahakama iliagiza afanyiwe uchunguzi huo pamoja na kuzuiliwa kwa siku nne ili kuwapa polisi muda wa kukamilisha uchunguzi
-Wazir alikamatwa na maafisa wa Kenya na Tanzania alipokuwa akielekea Zanzibar
-Alidaiwa kula uroda na wabunge 13 wanawake na kuwa na video iliyoonyesha uhondo wake na wabunge hao
-Wazir atashtakiwa kwa makosa mengi ikiwemo kuwatapeli watu na kutumia habari za watu wengine kutekeleza uhalifu
Mshukiwa aliyedaiwa kuwatapeli wabunge na Wakenya kwa kuwaibia fedha Benson Wazir Chacha atazuiliwa kwa siku nne ili kuwawezesha polisi kukamilisha uchunguzi, mahakama iliamuru Jumanne, Aprili 3.
TUKO.co.ke ina habari kuwa mahakama pia iliagiza kuwa Chacha mwenye umri wa miaka 23 afanyiwe uchunguzi wa kiakili katika hospitali ya watu wenye akili punguani ya Mathari baada ya mawakili wake kudai kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine: Vera Sidika atangaza hadharani kuwa ni mjamzito

Habari Nyingine: Askofu anusurika ‘kichapo’ kanisani Jumapili ya Pasaka
Katika kesi dhidi ya Chacha iliyosikilizwa na hakimu mkuu Christine Njagi, afisa wa uchunguzi, inspekta John Kipruto aliiambia mahakama kuwa walihitaji muda zaidi kukamilisha uchunguzi na kutafuta ushahidi zaidi dhidi yake.
Hata hivyo, wakili wa Chacha, Job Geresa alipinga ombi hilo, akidai kuwa haikuwa haki kwa mteja wake ambaye alidai kuwa alikuwa na uvimbe kwenye sehemu ya ubongo wake.
Habari Nyingine: Unamjua vyema mwakilishi wa kike wa Murang’a Sabina Chege?

Mshukiwa huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Central na kesi yake itaendelea kusikilizwa Jumatatu, Aprili 9.
Kama ilivyoripotiwa na TUKO.co.ke, tapeli huyo alikamatwa eneo la Tarime, Tanzania kwa msaada wa ujajusi wa maafisa wa Kenya na Tanzania.
Habari Nyingine: Lori la polisi lakamatwa likisafirisha magunia 120 ya makaa

Chacha ambaye ni mfanyikazi wa zamani wa wizara ya ugatuzi aliwatapeli viongozi wengi na kuwaibia pesa kwa kutumia jina la mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Murang’a Sabina Chege.
Kulingana na polisi, mshukiwa huyo amekula uroda na zaidi ya wabunge 13 wa kike.
Read ENGLISH VERSION
Una taarifa moto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News
Kutana na Vivian aliyepiga kibao ‘Chum Chum’ | TUKO TV
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibH1zgJZmpKygpaC2uK2MmqOisZWsrrWtz56jomWnlq%2B2usaeZKeZXaDCra2MrqmonJFiu6J51pqZrqaXmnpyf4ywmGajmaCybrfUn5insZmsrm7BwqGsp5%2Blr7Zuw8BmoqKZm565qnrHraSl