Kumbe kiranja wa maadili Kenya naye ni mfuasi wa kundi tata la Facebook!

Posted by Reinaldo Massengill on Tuesday, August 20, 2024

– Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu na Uratibu Kenya (KFCB), Ezekiel Mutua, ametoa maoni yake kupitia ukurasa maarufu sana wa Facebook wa kundi la Kilimani Mums

– Mutua anasema kundi hilo linahitaji nafasi ya uwaziri na kumtaka Rais Uhuru Kenyatta kulitilia maanani ombi lake

– Anasemna kundi hilo linawawakilisha Wakenya wa matabaka mbalimbali na hujadili masuala ambayo ni muhimu sana kwa jamii

– Kinaya ni kwamba, kundi hilo huzungumzia sana masuala ambayo Mutua huenda akasema hayafai kuwekwa hadharani

Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu na Uratibu Kenya (KFCB), Ezekiel Mutua, amechangia maoni yake kupitia ukurasa tata wa Facebook unaomilikiwa na kundi la Kilimani Mums

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Alhamisi Januari 18, Mutua anasema, ni bora ikiwa Rais Uhuru Kenyatta atalipa kundi hilo nafasi ya kiti cha Waziri.

"Nahisi Rais ni bora kulipa kundi hili lenye ucheshi nafasi ya Uwaziri," Mwenyekiti wa KFCB anasema kwenye ujumbe wake ambao TUKO.co.ke imeusoma.

Habari Nyingine:Bintiye Gavana Nyong'o - Zawadi Nyong'o - apiga picha akiwa uchi wa mnyama

Mutua anasema kundi la Kilimani humpa kila sababu ya kulifuatilia kwa kuwa humpasha kila analohitaji kufahamu na anashangaa ni vipi Wakenya waliishi kabla ya kundi hilo.

Habari Nyingine: Mwanamume akwama 'mvunguni' akila uroda na mpango wa kando

"Wakenya walikuwa wakiishi vipi kabla ya kurasa hizi? Watu huzungumzia kila suala," Mutua anasema.

Mutua amefurahishwa na kundi la Kilimani Mums kwa uwezo wake wa kuwaleta pamoja Wakenya wa kila tabaka.

Mwenyekiti huyo wa KFCB amelipongeza kundi hilo kwa kuwa na mchango bora na unaoweza kuchangia mabadilo katika sera za nchi.

Habari Nyingine:Je wanaume wanahitaji nini katika uhusiano? Wakenya watoa maoni yao

Ezekiel Mutua, anafahamika mno kwa makini yake katika kukabiliana na kituo chochote cha redio na Televisheni, ambavyo havizingatii maadili ya kijamii wakati wa kuendesha programu zake Kenya.

Kinaya ni kwamba, kundi hilo huzungumzia sana masuala ambayo Mutua, huenda akasema hayafai kuwekwa hadharani wakati yakijadiliwa kupitia redio ama Televisheni.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4B3fZZmoq6lkpp6rLXRmqWjmV2srm65wJqboqSZYrimutiaZKeZqZp6r7WMpp2umaOeeritjKSsp5yZYsGiwMBmo5pllpawpq7OqKJnoKSiuQ%3D%3D