Gavana Joho aongea baada ya maswali kuhusu cheti chake cha kidato cha nne

Posted by Aldo Pusey on Sunday, September 22, 2024

- Gavana wa Mombasa ameongea kwa mara ya kwanza baada ya maswali mengi kuhusu cheti chake cha kidato cha nne

- Baraza la mitihani la kitafa lilidai kuwa Hassan Joho hakufanya mtihani wake mwaka wa 1992

- Maswali pia yaliuliza kuhusu alama aliyopata Joho katika mtihani wa kitaifa KCSE

Gavana wa Mombasa Hassan Joho ametakiwa kufika mbele ya naibu wa kamishna wa polisi Mombasa kuhusiana na uchunguzi unaofanywa dhidi yake kwa madai kuwa aligushi cheti chake cha kidato cha nne.

Habari Nyingine: Huyu ndiye mtangazaji MREMBO zaidi nchini (picha)

Hassan Joho aliandika kwenye mtandao wake wa Facebook kuwa atauitikia wito wa naibu kamishna wa polisi kaunti ya Mombasa Jumatano Machi 29.

“Vitisho vinazidi kuniandama na jioni hii nimepata barua inayonihitaji kujiwasilisha mbele ya naibu wa kamishna wa polisi Mombasa.Nimewaeleza kuwa nina shughuli na hivyo basi nitaitikiwa wito wao siku nyingine” Joho alisema.

Habari Nyingine: Kisa hiki ni funzo kwa wanawake walio na tabia ya 'KUIBA' mabwana wa wanawake wengine (picha)

Shirika la ujasusi nchini limekuwa linachunguza uwezekano wa Hassan Joho kugushi cheti chake cha kidato cha nne.

Pata HAPA habari za TUKO.co.ke punde tu zinapochapishwa!

Kumekuwa na maswali mengi kuhusu alama kamili aliyopata Joho huku kukiwepo na vyeti viwili tofauti vinavyoonyesha alama tofauti.

Cheti cha kwanza kinaonyesha Haasan Joho alifanya mtihani wa KCSE mwaka wa 1992 katika shule ya upili ya Serani na kupata alama ya C+.

Habari Nyingine:Joho avamiwa na kurushiwa MAEMBE mabichi Lamu (video)

Cheti kingine kinadai kuwa alifanya mtihani huo huo mwaka wa 1993 katika shule hiyo na kupata alama ya D-.

Shirika la mitihani ya kitaifa KNEC liliandika barua kwa shirika la ujasusi na kusema kuwa Joho hakuwaifanya mtihani wake wa kitaifa 1992.

Subscribe to watch new videos

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: aron.mtunji@tuko.co.ke

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaIJxhZBmnpqukaOubrbOoaZmmZ%2BjtKatjJuYmpyRYsaiecyaqrCZnJ56rMHHrqquZZOdsrW1jJyfmqOVYrCprYykoJ2ZpKR6pLTAZqWnnV6dwa64